Ggavana wa bot hajafungua akaunti ya “facebook”

Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
inapenda kuutangazia umma kwamba Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.
Florens Luoga, hajafungua akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook,
kinyume na taarifa na picha zinazojitokeza katika katika mtandao huo kwa
jina lake. 
Kwa taarifa hii, tunapenda
kuutangazia umma kupuuza chochote kinachopatikana katika akaunti hiyo
bandia inayojiita Florence Luoga, na ambayo inatumia picha mbalimbali za
Gavana wa BoT kinyume cha sheria. 
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
inapenda kuwapa pole watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine
wameathirika kutokana na yote ambayo yamejitokeza katika akaunti hiyo
bandia, ikiwemo kutumia jina la Gavana Luoga kutapeli na hata kutumiwa
ujumbe wa matusi. 
Pamoja na taarifa hii, hatua za
kisheria zinaendelea kuchukuliwa ili kumbaini mhalifu huyu kwa kutumia
akaunti hiyo kuchafua sifa ya Gavana Luoga katika jamii. 
Tunauhakikishia umma kwamba,
Gavana Luoga hajafungua akaunti kwa jina hilo na hivyo taarifa zozote
zinazotolewa kwenye akaunti hiyo ya Facebook hazina uhusiano wowote na
Prof. Florens Luoga.