Icnl, apc yakutanisha waandishi wa habari arusha katika mafunzo ya uhuru wa kujieleza

Na Mwandishi Wetu, Arusha 
Waandishi wa habari wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kuripoti taarifa mbalimbali za mahakama za kimataifa ili kuuhabarisha umma kuhusu matukio yanayoendelea katika mahakama hizo.
Washiriki wa mafunzo kuhusu uhuru wa habari wakiwa katika majadiliano ya vikundi

Mshauri wa sheria wa shirika la ICNL Aloyce Habimana akiwasilisha mada kuhusu sheria zinazosimamia uhuru wa habari katika mafunzo yanayoendelea jijini Arusha kwa wanahabari

Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari wanaoripoti taarifa za mahakama za kimataifa ya Haki za watu na Binaadam (AfCPHR), pamoja na Mahakama ya Haki za binaadam ya Afrika Mashariki (EACJ), Afisa Habari Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika ya watu na Haki za binaadam Suckhdev Chatbar amesema waandishi wamekuwa kiungo muhimu sana katika mahakama hizo.


Afisa Programu katika taasisi ya wanasheria ya Pan African Lawyers Union (PALU),  Nelson Ndeki akieleza taasisi hiyo inavyofanyakazi hususani katika kutetea taasisi au wafungwa wanaofikisha mashauri yao katika mahakama za EACJ na AfCPHR.
Amesema waafrika wanapaswa kujua mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiendelea katika mahakama hizo hivyo ni jukumu la waandishi wa habari kutembelea katika mahakama na kuripoti kile kinachoendelea.
Chatbar ambae ameyazungumza hayo katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la International Center for Not for Profit Law ( ICNL) lenye makao yake makuu nchini Marekani,  kwa waandishi wa habari katika jiji la Arusha amesema AfCPHR  imekuwa ikiwakaribisha waandishi kila mara kuripoti taarifa za mahakama hiyo na wamekuwa wakifanya vizuri.

Amesema taarifa za waandishi zimekuwa zikitoa mchango mkubwa kwa jamii za mataifa mbalimbali Afrika ambao wamekuwa wakifikisha mashauri yao katika mahakama hiyo baada ya kutoridhishwa na mahakama katika nchi zao.