Jowuta yapata viongozi wapya, gwandu wa apc aukwaa uenyekiti

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jowuta wakifuatilia harakati za uchaguzi zikiendelea katika ukumbi wa maktaba ya Mkoa wa Dodoma
Wajumbe wakifuatilia uchaguzi
Viongozi wateule wakisikiliza mmoja wa wajumbe ambaye haonekani pichani
Mwenyekiti wa JOWUTA Claud Gwandu akitoa shukrani zake mara baada ya kuchaguliwa, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Jowuta Suleiman Msuya na kulia kwa Mwenyekiti ni Makamu Mwenyekiti Ramadhan Libenanga  na anayefuatia ni Mwekahazina Maurine Odongo na wa mwisho ni Naibu Katibu Mkuu, Said Mmanga
Makamu Mwenyekiti wa Jowuta Ramadhan Libenanga akitoa nasaha zake mara baada ya kuchaguliwa
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jowuta kutoka Mikoa na Majiji Mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliochaguliwa

gspot.com/-Nm9q8-047H0/XeiThKMdAHI/AAAAAAAABV0/x3URnreqShIWFe3vGovXkvE8CxBcIM5QwCLcBGAsYHQ/s640/IMG-20191130-WA0020.jpg” width=”640″ />

NA MWANDISHI WETU, DODOMA
CHAMA
cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania  (JOWUTA), kimepata
viongozi wapya ambao watadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Uchaguzi
huo umefanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma jijini
hapaambao wanachama 48 walishiriki kati ya 61 waliothibitisha kushiriki.
Mwenyekiti
wa Uchaguzi huo Keneth Ngelesi alitangaza washindi katika uchaguzi huo
ambapo nafasi ya Mwenyekiti mshindi ni Mwandishi Mkongwe Claud Gwandu
aliyeibuka mshindi kwa kura 30 dhidi ya Sitta Tuma aliyepata kura 17.
Ngelesi
alitangaza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa na mgombea mmoja
Ramadhan Libenanga ambaye alipata kura 43 za ndio na nne hapana.
“Nafasi
ya Katibu Mkuu wa JOWUTA mshindi ni Suleiman Msuya kwa kupata kura 44
za ndio tatu hapana na moja iliharibika na Said Mmanga amechaguliwa kuwa
Naibu Katibu Mkuu kwa kupata kura 46 za ndio na mbili za hapana,”
alisema.
Mwenyekiti huyo
alisema katika nafasi ya mweka hazina wajumbe walimpigia kura 47 za ndio
Maurine Odunga kuendelea kushika nafasi hiyo huku kura moja ikiwa ya
hapana.
Ngelesi alisema wajumbe waliwachagua Veronica Ignatus, Mussa Juma na Saphia Ngalapi kuwa wadhamaini wa chama.
Akizungumza
baada ya uchaguzi Mwenyekiti mpya wa JOWUTA, Gwandu alisema mafanikio
ya chama hicho yatatokana na wanahabari wenyewe kukijenga.
Gwandu aliwaomba waandishi wote nchini kutumia chombo hicho kupigania haki, maslahi  na maendeleo yao na nchi.
“Nawaomba
wenzangu tushitikiane kuijenga JOWUTA na ili hilo lifanikiwe ni wajibu
wa kila mmoja kutafuta wanachama kuanzia 10 wajiunge tuende pamoja kudai
haki zetu kisheria,” alisema.
Mwenyekiti
hiyo aliwataka wanachama wajitahidi kulipa ada ya kila mwezi ili
kuwezesha chama kujiendesha chenyewe na kufuatilia stahiki za waandishi
kisheria.
Mbali na uchaguzi wa viongozi mkutano huo ulifanya mabadiliko ya kiingilio kutoka shilingi 5,000 na kuwa shilingi 10,000/.
JOWUTA
ilisajiliwa mwezi Machi mwaka jana ambapo kwa sasa kina wanachama zaidi
120  katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tabora, Arusha,
Mbeya na Mwanza.
Uchaguzi
huo umefanyika baada ya Jowuta kuwa chini ya uongozi wa muda ambapo
Said Mmanga alikuwa Mwenyekiti, Saphia Ngalapi, Makamu Mwenyekiti,
Samson Kamalamo, Naibu Katibu Mkuu na Maureen Odunga, Mwekahazina.
Jowuta
ilisajiliwa Machi, 2018 baada ya Mahakama Kuu, kitengo cha Kazi
kukifuta kilichokuwa Chama cha Wafanyakazi Waandishi wa Habari Tanzania
(TUJ), mwaka 2014, kufuatia maombi ya msajili wa vyama vya wafanyakazi
na waajiri.