Kampeni ya utatu yazinduliwa…mkuchika asema kila mtanzania ana jukumu la kupambana na rushwa

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utwala Bora, Kapteni, George Mkuchika
amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali katika kupambana na Rushwa
ili kupunguza ajali za barabarani pamoja na kuwezesha upatikanaji wa
haki kwa wananchi.

Akizungumza
katika uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia rushwa barabarani Waziri Mkuchika
amasema kuwa katika kampeni hiyo ijulikanayo kama “Utatu inayohusisha
Taasisi ya kuzuia na Kupambana  na Rushwa Takukuru, Jeshi la Polisi na
Wananchi inawezekana na itasaidia katika kutoa taarifa za rushwa
zishughulikiwe kwa haraka ili kupunguza ajali barabarani.

“ Nyote mtakubaliana na mimi kuwa jukumu la kupambana na rushwa
lilikasimiwa kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru, ili
kukabiliana na vitendo vya Rushwa vinavypatikana katika maeneo yetu,kila
mmoja wetu anapaswa kubeba jukumu la kupambana kama kampeni hii
inavyoeleza”, alisema Waziri Mkuchika.
Alisema kuwa mara nyingi vitendo vya rushwa vinafanyika pale ambapo watu
wanafanya kazi, wanafanya biashara, wanapata huduma na kwenye makazi
kwa hiyo inawezekana kwa kila mtu kuchukua jukumu la kuzuia rushwa kwa
sababu inatokea kwenye maeneo ambayo wananchi wanahusika,wanaisikia na
kuona vitendo hivyo katika mazingira tofauti.
Waziri Mkuchika alieleza kuwa iwapo kila mtanzania atachukua dhamira ya
dhati ya kuiunga mkono Serikali katika mapambano hayo, ajali za
barabarani zitapungua, kwani mpaka sasa takwimu za mwaka 2018/2019
zinaonesha kuwa ajali za barabara zimepungua kwa kushirikisha wadau,
Polisi na Taasisi ya kupambana na rushwa Takukuru.
Aidha Waziri Mkuchika amezindua Mfumo wa kitekenolojia unaoitwaTakukuru
App unaopatikana kwenye simu ambao utatumika kuripoti vitendo vya Rushwa
katika maeneo mbalimbali nchini.
“Mfumo huu ni mzuri kwani unamuwezesha mwananchi kukusanya taarifa na
matukio ya vitendo vya rushwa kwa kutumia simu ya Mkononi na kuwasilisha
kwa takukuru au jeshi la Polisi  ambapo zitafanyiwa kazi na mtuhumiwa
kufikishwa sehemu husika”, Alisema Waziri Mkuchika.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amesema
kuwa Serikali inatakeleza jukumu kubwa la kuleta usawa wa haki kwa
wananchi nchini kwa kupambana na rushwa ikiwemo ufisadi ili kuleta
maendeleo kwa wananchi, kwa hiyo Jeshi la Polisi linaunga mkono jukumu
hilo ambalo linafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli.
“ Mchakato wa kampeni hii ni sehemu ya matakwa ya kihistoria na
kitaasisi katika jitihada za kupambana na rushwa nchini iliyoanzishwa
chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kifungu namba 11 ya
mwaka 20007, sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa sheria ya kuzuia
rushwa ya Takukuru sura 329 ambayo ilifanyiwa marejeo mwaka 2002, kwa
hiyo katika kutekeleza majuku haya kampeni hii ambayo mchakato wake
ulianza Novemba, 2017 leo inazinduliwa itasaidia sana kupunguza ajali
barabarani”, Alisema IGP. Sirro.