Kingwalla: “walipanga kuniangamiza na walitaka nitumbuliwe uwaziri”

Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, ameeleza kuwa kwa sasa
anaishi kwa hofu na tahadhali kubwa juu ya uhai wake kutokana na kuwepo
kwa kundi la watu wanaomuwinda wakitaka kumuangamiza huku wengine
wakimfanyia mipango ya kumuharibia ili atumbuliwe uwaziri.


Kupitia
akaunti yake ya instagram Kigwangala ameweka wazi kuwa hata alivyopata
ajali aliwekewa ulinzi mkali wodini ili wabaya wake wasiweze kummalizia
kwa namna yoyote.

Kupitia instagram yake ameandika hivi; Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. 

Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. 

Bahati
mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na
kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro
wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama.
Sikukaidi. 

Wakaona
wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo,
tutakutana mahakamani ambapo mbivu na mbichi zitajulikana, ukweli
utawekwa wazi na rekodi itakaa sawa. Sijashangaa kuwa wahusika ni wale
wale wa kipindi kilichopita.


Hakuna
jipya. Sababu ni deal yao binafsi, ambayo haitekelezeki bila ridhaa ya
Waziri, na bahati mbaya kwao Waziri ni mimi; walitamani nisiwepo
watafune pesa za serikali vizuri, wamekwama. 

Tutaendelea
kudhibiti kimya kimya. Kwa wanaokumbuka wakati nimelazwa ICU na baadaye
wodini, ilikuwa ngumu sana kunitembelea na kuniona. 

Paliwekwa
ulinzi mkali sana na watu wote walizuiliwa kuingia isipokuwa kwa kibali
cha Ikulu, hadi Mawaziri wenzangu hawakuruhusiwa. 

Nilishangaa
sana lakini niliambiwa ndiyo hivyo. Baadaye nikaja kujua kuwa kuna watu
walipanga njama za kuniua na hiyo ingeweza kuwa fursa kwao
kunimalizia. 

Baada
ya kuteuliwa tu Wizara hii kulizuka mtafaruku mkubwa sana juu ya
usalama wangu, nilifuatiliwa kila kona mpaka serikali ikanipa walinzi,
nilibisha kwa kuwa sipendi attention sana lakini nililazimishwa na
kuambiwa nipo kwenye ‘threat’! Sikuwa na option. 

Nilianza
kuishi kwa hofu na mashaka sana. Hivyo, baada ya ajali na yaliyotokea
kutokea nililazimika kuwa makini zaidi. Imani yangu kwa kila mtu
ilipungua. Nikawa ‘alert’ wakati wote. 

November
2019 nililetewa taarifa za kutisha, nikaongeza umakini. Team yangu
imenisihi nisiweke majina hadharani na kwamba wanawafuatilia wahusika
kwa ukaribu na watazijulisha mamlaka kwa hatua stahiki zaidi. Watu wa
karibu sana na mimi nimewapa mpango na taarifa zote na wanajua cha
kufanya endapo chochote kitanitokea. Kuna mbinu nyingi za mapambano.
Tuendelee tu!