Kkkt yaipongezaserikali kwa kuleta maendeleo na kutoa ushirikiano katika hudumaza kijamii nchini

Na James Mwanamyoto, Njombe

Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) limeipongeza Serikali kwa kuleta maendeleo katika miundombinu
ya barabara, reli na anga, kuhimiza maendeleo ya viwanda ili kuwawezesha
watanzania kuuza bidhaa zilizoandaliwa, ikiwa ni pamoja na kutoa uhuru wa kila
mtanzania kuabudu.

Pongezi hizo zimetolewa na
Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango mara
baada ya kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Ibada Takatifu
iliyofanyika jana Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Baba Askofu Dkt.
Frederick Shoo.

Askofu Fihavango amesema,
Kanisa linaishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Dayosisi yake hususani
katika sekta ya afya.

Dayosisi yangu ina ubia na
Serikali wa kutoa huduma za afya kupitia Hospitali Teule ya Kilutheri Ilembula
iliyopo Wangingombe ambapo kati ya watumishi 182 waliopo, Serikali inalipa
mishahara watumishi 110 kupitia mfuko wa ruzuku, amefafanua Dkt. Fihavango.

Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George
Mark Fihavango akiipongeza Serikali kwa kuleta maendeleo nchini mara baada ya
kusimikwa kuwa askofu wa Dayosisi hiyo katika Ibada takatifu iliyofanyika
Mjini Njombe na
kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimuwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ibada ya
kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark
Fihavango iliyofanyika
Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu
Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani)
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na
madhe
hebu mengine wakishiriki ibada ya kumsimika Askofu wa
Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika
Mjini Njombe na
kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani) 
Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo akimpongeza Mhe. Rais, Dkt.
John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kuwaletea watanzania maendeleo,
pongezi hizo
amezitoa mbele ya waumini wa KKKT na madhehebu mengine
wakati wa ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt.
George Mark Fihavango iliyofanyika mjini Njombe

Askofu  Fihavango ameongeza kuwa, Serikali imekuwa
ikitoa fedha na vifaa tiba kwenye hospitali hiyo ili kuwezesha utoaji wa huduma
bora za matibabu kwa wananchi, akitoa mfano katika mwaka wa fedha 2018/19
hospitali imepokea jumla ya shilingi 187,421,791/=
na ruzuku ya mishahara ya watumishi kiasi cha shilingi 1,056,168,000/=.


Kama haitoshi, Askofu
Fihavango ameeleza kuwa, Serikali imetoa gari la wagonjwa kwa Hospitali ya
Kilutheri Ilembula na Kituo cha Afya Kidugala ambalo limesaidia kuboresha
huduma za afya hasa za mama na mtoto hivyo inaonyesha dhahiri kuwa kanisa na
Serikali ni washirika katika kuleta maendeleo ya taifa.

Akimuwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ibada hiyo, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.
(Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametoa pongezi kwa KKKT kwa kushirikiana na
Serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Mhe. Mkuchika amesema,
Serikali inatambua mchango wa kanisa hilo katika kutoa huduma za kiroho, afya,
elimu na uchumi bila kubagua wananchi kwa kigezo cha utofauti wa dini, hivyo
limekuwa na mchango katika maendeleo ya taifa na kulitaka kuwahimiza waumini
wake kutokwepa kulipa kodi ili Serikali ipate fedha za kuendesha shughuli za
maendeleo.

“Katika kutoa huduma za afya,
Serikali inaendelea kushirikiana na kanisa kutoa huduma hiyo kupitia Hospitali
Teule ya Ilembula na Kituo cha Afya Kidugalo na zahanati nyinginezo ambazo ni
mali ya KKKT Dayosisi ya Kusini” Mhe. Mkuchika ameongeza.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa
Serikali inatoa vifaa tiba na mishahara kwa watumishi wa Hospitali Teule ya
Ilembula ambao 110 ni wa kanisa na 37 wa Serikali ili kuwawezesha wananchi
kupata huduma bora za matibabu.

Aidha, Mhe. Mkuchika ametoa
wito kwa KKKT kuendelea kushirikiana na Serikali katika kushauriana na
kudumisha utamaduni wa kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ustawi na
maendeleo ya wananchi kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa KKKT,
Askofu Dkt. Frederick Shoo amempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli na Serikali yake kwa kuwaletea watanzania maendeleo katika sekta ya afya,
elimu na nishati.

Askofu Dkt. Shoo, pia hakusita
kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kurejesha nidhamu ya utendaji kazi katika
utumishi wa umma kwani nidhamu ya watumishi wa umma imekuwa ni chachu ya
maendeleo katika taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H.
Mkuchika (Mb) amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye
Ibada ya kumsimika Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini, Dkt. George Mark
Fihavango iliyofanyika Njombe, Oktoba 13, 2019.