Mkurugenzi
wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji Simon Nkanyemka katikati akimsikiliza
kwa umakini Mhandisi wa Miradi Tanga Uwasa Mhandisi Salum Ngumbi
kushoto akielezea mradi unaotoa maji Pongwe kuelekea Muheza wakati wa
ziara hiyo katikati Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na
kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
MKURUGENZI
wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji Simon Nkanyemka kushoto akiteta jambo
na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati
alipotembelea mradi wa maji wa kutoa maji Pongwe kwenda wilayani Muheza
uliopo eneo la Kilapula Jijini Tanga wakati wa ziara yake katikati ni
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
MKURUGENZI
wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji Simon Nkanyemka wa pili kutoka kulia
aliyevaa shati jeupe kuwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey
Hilly wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wengine wakati wa
ziara ya siku mbili ya kukagua na
kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji pamoja na kubaini changamoto
zake .
MENEJA wa Ruwasa wilaya ya Lushoto Eron Sizinga akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo kulia ni MKURUGENZI
wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji Simon Nkanyemka
MKURUGENZI
wa Huduma
za Sheria Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka kulia akisistiza jambo katika
mradi wa maji wa Shume-Manolo-Madala wilayani Lushoto wakati wa ziara
yake
ya siku mbili ya kukagua na kufuatilia
utekelezaji wa miradi ya maji pamoja na kubaini changamoto zake
mkoani Tanga wa kwanza kushoto aliyevaa chekundu ni Meneja wa
Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akifuatiiwa na Meneja wa
Ruwasa wilaya ya Lushoto
Eron Sizinga
MKURUGENZI wa Huduma
za Sheria Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka aliyevaa shati jeupe na suruali nyeusi katika akimsikiliza Meneja RUWASA Wilaya ya Korogwe, Sifael Massawe
akimueleza jambo wakati alipotembelea chanzo cha maji
MKURUGENZI
wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji Simon Nkanyemka amewashauri mameneja wa
Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) kote nchini kwenda vijijini kutoa elimu kwa
jamii umuhimu wa uchangiaji wa huduma za maji kama inavyoelekeza sheria ya maji namba
5 ya mwaka 2019.
Saimon alitoa ushauri huo jwilayani Muheza wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku mbili ya kukagua na
kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji pamoja na kubaini changamoto zake .
Alisema sheria ya Maji namba 5
ya 2019 inaeleza wazi kuwa miradi ya maji vijijini inatakiwa kuendeshwa na
wataalamu waliosoma kupitia bodi za maji ikiwemo wananchi kuchangia huduma ili
miradi iweze kuwa endelevu
“Hivyo kutokana na ziara yangu
nimegundua wananchi wengi bado hawana uelewa juu ya sheria hii haswa katika
suala la uchangiaji wa huduma haiwezekani kwa mwezi mtu analipa Sh 500 tu mameneja
RUWASA nendeni kwenye miradi ya maji vijijini mkawaelimishe Wananchi”Alisema
Nkanyemka katika ziara hiyo aliambatana na Maofisa kutoka Bonde la Mto Pangani na
Mtaalamu wa Ubora wa Maji kutoka Wizara ya Maji pamoja na Meneja RUWASA mkoa wa
Tanga,Upendo Lugongo alitembelea miradi ya maji katika wilaya za
Korogwe,Lushoto na Muheza pamoja na kukagua chanzo cha maji cha bonde la Mto
Zigi.
Akiwa wilayani Korogwe alitembelea
mradi wa Maji wa Mtonga-Msambiazi ambao unatoa huduma za maji katika
vijiji vya Mtonga,Majengo na Msambiazi mradi ambao umegharimu fedha kiasi cha
Sh milioni 595 ambapo changamoto aliyokumbana nayo ni mradi huo kukamilika
lakini maji yanatoka kwa mgao kutokana pampu kubwa iliyofungwa kwa ajili
ya kusukumia maji haijaanza kazi kutokana Shirika la Umeme(Tanesco) wilayani
humo haijafunga mita kubwa ya kuiwezesha pampu hiyo kufanya kazi.
Vile vile alitembelea kituo cha
maji katika kijiji cha Msambiazi ambacho kinapata maji kupitia mradi huo
huku akikutana na malalamiko ya wananchi kuyalalamikia maji hayo kuwa yana rangi hali
ambayo wananchi wameamua kuyatumia maji hayo kwa shughuli nyingine za nyumbani
lakini si kwa matumizi ya binadamu.
Kufuatia malalamiko hayo,Nkanyemka alimuagiza Meneja RUWASA Wilaya ya Korogwe, Sifael Massawe
kuhakikisha Tanesco wanafunga mita hiyo ili kuondoa kero ya mgao wa maji pamoja
na kuwatoa wananchi hofu kuwa maji hayo ni salama kwa matumizi ya
binadamu na serikali itahakikisha kupitia wataalamu wa Wizara ya Maji wanaondoa
rangi hiyo.
“Kupitia mradi mkubwa
wa maji wa HTM ambao utatoa huduma za maji katika wilaya za
Muheza,Handeni,Korogwe na Pangani kupitia chanzo cha mto Pangani ambao
utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu, kutawekwa mtambo
wa kuchuja maji,hali hii haitajitokeza tena serikali haitakubali kuwaletea maji
yasiyo salama,yaliyopo ni salama tatizo ni rangi tu lakini yamepitia hatua
mbalimbali za kuchuja,”alisema.
Hata hivyo kwenye wilaya ya Lushoto
alitemebea mradi wa maji wa Shume-Manolo-Madala ambao unahudumia vijiji sita
katika kata ya Manolo jimbo la Mlalo na wananchi 35,000 alitembelea tenki la
kuhifadhia maji na kituo cha maji katika kijiji cha Nyolwe ambapo alikumbana na
wananchi kulalamika kupata maji kwa mgao na wananchi wanataka kuchangia huduma
ya maji kwa gharama ya Sh 500 tu kwa mwezi kwa kila kaya.
Akizungumzia suala hilo,Meneja Ruwasa Wilaya ya Lushoto,Eron Sizinga alisema kuwa mradi
huo una matenki mawili na vituo 71 ambavyo vinahudumia katika vijiji
sita,na maji hayo yanatoka kwa mgao kutokana bado mradi upo katika hatua ya
majaribio ya mkandarasi haujakabidhiwa kwa uongozi wa RUWASA ndio maana maji
yanatoka kwa mgao mara moja au mbili kwa wiki kwa kila kijiji.
Wilayani Muheza alitembelea
mradi wa maji wa Mashekiwasa ambao unahudumia vijiji vitatu vya Kimbo, Mashewa
na Shembekeza ambapo pia alikumbana na changamoto ya wananchi kugoma kulipia
huduma hizo za maji zaidi ya Sh 500 kwenye vituo na Sh 1000 kwa wale
waliounganishiwa huduma hadi nyumbani.
Katika hatua nyingine,amepongeza
hatua ya uhifadhi wa chanzo cha maji katika mto Zigi kupitia mradi wa uhifadhi
wa vyanzo vya maji katika mabonde ya Ruvu na Zigi na kusema kuwa matokeo ya
uhifadhi huo ni mfano wa kuigwa katika vyanzo vingine vya maji.
Katika mradi huo,wananchi
wanaoishi kandokando ya vyanzo vya maji wamepewa elimu ya kupanda mazao mbadala
ambayo hayaharibu vyanzo vya maji ambapo wananchi wameweza kuzingatia na
kutunza vyanzo hivyo ambapo kiwango cha maji katika mto Zigi kimeongezeka
kutoka mita 4.3 hadi mita 6.5 katika kipindi cha miaka mitano tangu mradi
uanze.
Mafanikio mengine ni kupungua
kwa kiwango cha mchanga ndani ya mto kutoka kilo 1.4 kwa eneo la mita za mraba
hadi kilo 0.49 kwa eneo la kilometa za mraba pamoja na kuinua kiwango cha
maisha ya wananchi kupitia miradi mbadala ya kiuchumi na kuongeza kwa
uelewa kwa wananchi juu ya uhifadhi vyanzo vya maji.
Mradi huo wa uhifadhi vyanzo vya
Maji katika Bonde la Myo Zigi na Ruvu umefadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa
fedha kiasi cha Sh bilioni 11 na wanadu wa maenedeleo ambao ni Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) na GEF ambao kwa pamoja wametoa Sh 16.5
bilioni.