Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi
Macha amewataka wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, wakurugenzi wa
Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji wa idara ya Ardhi kwenda kutatua
migogoro ya ardhi kwa wananchi.
Ameyasema hayo leo katika hafla
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karena Hotel baada ya makabidhiano ya nyaraka na
ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
RC Macha amesisitiza viongozi hao kwenda
kutatua changamoto za ardhi ana kwa ana huku akiwahimiza kuendelea kutoa elimu
kwa wananchi ili waweze kufahamu mipaka na haki zao katika umiliki wa ardhi na
kwamba hatua hiyo itasaidia kuimarisha usalama kwa wananchi.
“Yapo
masuala ya migogoro ya Ardhi tukajipange kwenye Halmashauri na mashauri yetu
yanayohusu Ardhi ni vizuri tukaenda kuyafanyia kwenye eneo linalozozewa
tusiende ofisini kufanya maamuzi, sidhani kama tutaimaliza migogoro ya Ardhi
kwa kutatua tukiwa ofisini hiyo tutadanganyana nafikiri ofisi zetu za idara ya
Ardhi ziwe zinaenda kuweka kambi kwenye maeneo yenye changamoto ili kutatua
migogoro hiyo”. Amesema RC Macha
Amewataka wakurugenzi wa Halmashauri,
wenyeviti wa Halmashauri pamoja na wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia vema
suala la ukusanyaji wa mapato ili kuepusha changamoto mbalimbali ikiwemo wizi
ambapo amesema kuimarika kwa zoezi la ukusanyaji wa mapato itasaidia kwa kiasi
kikuwa kuchochea maendeleo.
Amesema
serikali itaendelea kuwahakikisha mazingira ya Amani,usalama na upatikanaji wa
huduma bora na stahiki za kijamii wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande naibu katibu Mkuu ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme amewaomba wananchi wa
Mkoa wa Shinyanga kushiriki vema kwenye
ajenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati
safi ya kupikia ili kutunza mazingira.
“Niwaombe wana Shinyanga katika ajenda hii ya
mazingira ifikapo Mwaka 2030 wanawake asilimia 88 wawe wanatumia nishati safi
ya kupikia lakini pia tuwe wa kwanza katika suala la utunzaji wa mazingira
lakini tuendelee kumuunga Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala hili la
utumiaji wa nishati safi ya kupikia na utunzaji wa mazingira”.amesema Mndeme
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga mpya Mhe. Anamringi Macha leo amekabidhiwa ofisi kwa ajili
ya utekelezaji wa majukumu yake ambapo amejitambulisha kwa viongozi mbalimbali
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga na kwamba siku
chache zimepita baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kufuatia
uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu
Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi
Macha akizungumza kwenye hafla hiyo leo Jumatatu March 18,2024 katika ukumbi wa
Karena hotel mjini Shinyanga.
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla hiyo leo
Jumatatu March 18,2024.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM
Mkoa wa Shinyanga Odilia Batibayo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) na Jaji mfawidhi wa
Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Frank Habibu Mahimbali upande wa kulia.
Aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Katibu
Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme upande wa kushoto akipokea
zawadi.
Aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Katibu
Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme akipokea

Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Janeth Magomi
akimkabidhi zawadi aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme

Kamanda
wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi
(SACP) Janeth Magomi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha

mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na
Muungano Bi. Christina Mndeme akipokea zawadi
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme wakiwa kwenye picha
ya pamoja leo March 18,2024 katika ukumbi wa Karena Hotel Manispaa ya
Shinyanga.