Picha : wanawake watia nia wapewa mafunzo kugombea na kushinda kwenye uchaguzi serikali za mitaa


Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya akizungumza katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka vitongoji na vijiji kwenye baadhi ya kata wilaya Kishapu mkoani Shinyanga.


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania ‘TGNP
Mtandao’ umetoa mafunzo ya uongozi kwa Wanawake,vijana na watu wenye
ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  kwenye
uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 ili
kuwajengea uwezo,ujasiri,mbinu na mikakati ya kuingia katika
kinyang’anyiro cha uchaguzi na kushinda.




Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo
Jumatano Oktoba 23,2019 kwenye ukumbi wa BM uliopo katika kata ya
Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na kukutanisha watia nia 65
kutoka baadhi ya kata za wilaya ya Kishapu.


Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Theresia Sawaya ambaye ni Mwanasheria kutoka
TGNP Mtandao alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo
wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea kwenye
uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kugombea na kushinda kwa
kishindo.

“Tumekutana na watia ni kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi
ili kuwafundisha kuhusu dhana za jinsia na namna zinavyotumika na athari
zake katika masuala ya uongozi lakini pia kuwajengea uwezo namna ya
kufanya kampeni kwenye uchaguzi,namna ya kupata rasilimali fedha na
ulinzi na usalama wa wagombea”
,alieleza Sawaya.


Alisema kupitia mafunzo hayo wanatarajia wanawake ambao katika miaka ya
nyuma wamekuwa nyuma kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi watahamasisha
na kupata ujasiri wa kugombea na kushinda katika uchaguzi na kushiriki
katika ngazi mbalimbali za maamuzi.


Kwa upande wake, Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa ambaye pia ni
mwezeshaji katika mafunzo hayo aliwataka wanawake watia nia kugombea
kwenye uchaguzi kuhakikisha wanawashirikisha waume zao ili kupata
matokeo mazuri zaidi.

“Wanawake tunapogombea madaraka ni vyema kuwashirikisha watu
wanaotuzunguka,washawishini waume zenu wawaunge mkono ikibidi muwaombe
wawe makampeni meneja wenu,wataongea na wanaume wenzao ili wawape kura
na mtapata ushindi mnono”,
alisema Juma.


Aidha aliwataka wazazi kutowabagua watoto kwa kuwapa kipaumbele zaidi
watoto wa kiume huku akisisitiza kuwa kama wazazi wawape majukumu sawa.

“Tuwafundishe watoto wa kiume kuacha kuwa tegemezi,tuwafundishe
kushirikiana na dada zao kufanya kazi wanazopewa nyumbani,kwani mtoto wa
kike siyo mfanyakazi wa nyumbani, mtoto wa kike anapaswa kupewa haki
sawa na mtoto wa kiume”
,alisema.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia
Sawaya akielezea kuhusu mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia ya
kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka
vitongoji na vijiji kwenye baadhi ya kata wilaya Kishapu mkoani
Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia
Sawaya ambaye ni Mwezeshaji katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake
watia nia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akiwahamasisha wanawake
kujiamini kwani wanaweza kuongoza jamii kutokana na kwamba mwanamke ni
kiongozi kuanzia ngazi ya familia.


Wanawake watia nia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwa ukumbini.

Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa
ambaye pia ni mwezeshaji katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia
nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akiwasisitiza kuepuka
rushwa ya ngono kwenye uchaguzi.

Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa
akizungumza wakati wa mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia
kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akiwasisitiza kuepuka
rushwa ya ngono kwenye uchaguzi.
Diwani wa Kata ya Mwadui Luhumbo,Mhe.
Sarah Masinga akiwatia moyo wanawake waliotia nia kugombea nafasi za
uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa wajiamini,wamtangulize
Mungu na kushirikiana na jamii ili kushinda katika nafasi wanazogombea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisiliza nasaha mbalimbali.


Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na
maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo akiwasisitiza wanawake kupendana
na kuacha tabia ya kukwamishana wao kwa wao.
Mtia nia ya kugombea nafasi za uongozi
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,Mary Richard Nzingula akizungumza
wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.

Mlezi wa wanawake watia nia ya kugombea
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wilaya ya Kishapu,Mhe. Suzana
Makoye ambaye ni Diwani wa Viti Maalum kata ya Maganzo akiwasisitiza
wanawake watia nia kutokata tamaa pale wanapokutana na changamoto
mbalimbali.
Picha zote na Kadama Malunde


Soma Pia : MWANASHERIA TGNP MTANDAO : WANAWAKE MSIKUBALI KUTUMIA MIILI YENU KUWEZESHWA KISIASA