Ahmed Mahmoud/Arusha
Naibu Katibu
Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Thembinkosi Mhilongo amesema umoja huo umedhamiria kuwa na VISA moja kwa lengo la kupunguza urasimu ndani ya Jumuiya
hiyo
Hayo
yameelezwa leo na Naibu Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC Dkt Thembinkosi Mhilongo wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana na Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii katika nchi hizo za Ukanda wa
Kusini mwa bara la Afrika (SADC).
Dkt Mhilongo
pia amesema nchi za SADC zimejipanga
kuangalia kwa kina suala la
Viumbe na Mimea vamizi katika nchi hizi
wanachama pamoja na Wanyama ambao wako katika hatari ya kutoweka
katika nchi hizo.
Naibu Mtendaji
Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao
wenye dhamana ya mazingira, maliasili na utalii kuhakikisha wanaangalia kwa kina Itifaki na Mikataba inayohusu Sekta hizo tatu katika nchi
Wanachama za SADC
Amesema Mkutano
wa Mawaziri hao ni muhimu katika kukuza na kuchangia katika ukuaji wa uchumi
wa mataifa ya SADC hivyo
amewataka wakati wa Mkutano huo kupima na kuangalia kwa kina Sera na Itifaki zinazosimamia Sekta hizo tatu ambazo ndio muhimili mkuu wa
Uchumi wa mataifa hayo.
Mbali na kuangalia
masuala hayo Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao
kuhakikisha wanaangalia kwa Kina Sheria zote zinazosimamia na kuongoza Sekta
hizo katika Jumuiya.
Amesisitiza
kuangaliwa upya Itifaki ya Utalii, Mazingira, na Maasili katika nchi Wanachama
za SADC na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na umuhimu kwa Mawaziri hao kuhakikisha majandiliano ya Mkutano wao yanalenga katika
kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mazingira, maliasili na Utalii katika
nchi za SADC
Nchi za SADC
imebahatika kuwa na raslimali lukuki
zikiwemo za Wanyamapori, misitu, Uvuvi
rasilimali ambazo ni muhimu katika
kuchangia ukuaji wa Uchumi na maendeleo ya nchi wanachama za SADC.
Amewataka
Mawaziri hao kuangalia kwa kinja Itifaki
ya SADC inayohusu umuhimu wa
kusimamia na kulinda uhifadhi, kuangalia Itifaki ya misitu, Uvuvi na Sheria ya usimamizi wa Wanyamapori
Pia
amesisitiza umuhimu kwa SADC Kutambua umuhimu wa kusimamia , kulinda na
kuhifadhi misitu ili kuwa na uhifadhi endelevu katika nchi hizi za Ukanda wa
Kusini mwa Afrika
Naibu
Mtendaji Mkuu huyo amesema Jiji na Mkoa wa Arusha limebeba historia
kubwa ya SADC kutokana na kuwa Jiji hili ndipo chimbo kubwa la
kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika miaka 40 iliyopita
Amesema SADC
iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Keneth Kaunda wa Zambia,
Rais Somora Machel wa Msumbiji, Rais Agustino Neto wa Angola na Rais Gabriel
Mugabe wa Zimbabwe ambapo Jumuiya hiyo iliasisiwa katika Ukumbi huo wa AICC
Aidha Mkataba
wake ulisainiwa Lusaka Nchini Zambia kwa
ajili ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambapo Makao ya SADC yapo Gaboro Nchini Botswana
Kukosekana kwa Visa moja kwa Watalii ulaya wanapokuja katika ukanda huu wa kusini mwa nchi za
kusini mwa Afrika ni moja ya changamoto kubwa
|