Spika pelosi aanzisha uchunguzi rasmi kuhusu madai ya ukraine yanayomuhusisha trump

Pelosi and Trump
Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrat Nancy Pelosi (kushoto)amesema kuwa rais Trump “lazima awajibike

Chama cha Marekani
cha Democrats kimeanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya rais wa nchi hiyo
Donald Trump kuhusiana na madai kwamba alitaka usaidizi kutoka kwa taifa
la kigeni ili kumuangamiza hasimu wake wa kisiasa.
Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrat Nancy Pelosi amesema kuwa rais “lazima awajibike “.
Bwana Trump anakanusha madai hayo na amezitaja juhudi za kumtuhumu kama ” hila chafu” dhidi yake .
Huku
kukiwa na uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wafuasia wa Democrats juu ya
uchunguzi huo unaoweza kumuondoa mamlakani, ikiwa utaendelea huenda
usipitishwe na baraza la seneti – linalodhibitiwa na wabunge wa chama
cha Trump cha Republican.
Mzozo huo ulichochewa na ripoti za jasusi aliyefichua
malalamiko kuhusu simu ambazo rais Trump alimpigia mwenzake wa Ukrain
rais Volodymyr Zelensky.


Kuhusu ni nini hasa alichosema limesalia kuwa
lisilo wazi , lakini Democrats wanamshutumu Bwana Trump kutishia
kusitisha msaada wa kijeshi kuishinikiza Ukraine kuchunguza madai ya
rushwa dhidi ya makamu wa rais wa zamani Joe Biden na mtoto wake wa
kiume Hunter.
Bwana Trump amekiri kuwa alimzungumzia Joe Biden
na Bwana Zelensky lakini akasema alkuwa tu akijaribu kuitaka Ulaya
iingilie kati kutoa msaada kwa kuitishia kusitisha msaada wa kijeshi.
Speaker of the House Nancy Pelosi
Awali Spika Nancy Pelosi alikataa kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya rais
Bi Pelosi amesema nini ?
Bi
Pelosi alisema kwua Bwana Trump amefanya kosa la “ukiukaji wa sheria
“, na kuyataja matendo yake kama “uvunjaji wa wajibu wake wa
kikatiba”.
“Wiki hii rais Trump alikiri kumuomba rais wa Ukraine
kuchukua hatua ambazo zitamnufaisha kisiasa ,” alisema, na kuongeza kuwa
: “Rais lazima awajibishwe.”
Kama Spika wa bunge, Bi Pelosi ni
afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Democrat. Bi Pelosi awali amekuwa
akipinga miito ya kutaka amuondoe madarakani rais wa Republican akidai
juhudi za aina hiyo zinaweza kuimarisha uungaji mkono kwa Trump.


Bwana Biden amekanusha kufanya kosa lolote na pia
anaunga mkono juhudi za kumfanyia upelelezi rais iwapo hataonyesha
ushirikiano katika sakata hiyo dhidi yake.
Uchunguzi dhidi ya
Bwana Trump “unaweza kuwa janga “, alisema Bwana Biden . “Lakini janga
alilojitengenezea mwenyewe .” Kwa sasa ndiye mtu aliyemstari wa mbele
katika kukabiliana na Bwana Trump katika uchaguzi wa 2020.
Trump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia)
Trump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia
Bwana Trump alijibu vipi ?
Katika
msururu wa jumbe zake za Bwana Trump alisema Democrats wana lengo la
“makusudi la kuharibu ” ziara yake katika Umoja wa Mataifa ” kwa
taarifa zaidi za hivi punde za hila chafu za takataka “.
“Hata hawajaona ujumbe ulioandikwa wa simu wanazodai nilipiga . Hila tupu !” aliongeza
Aliahidi
kutoa ujumbe wa mazungumzo baina yake na mwenzake wa Ukraine kwa
maandisi siku ya Jumatano ili kuonyesha kuwa “ulikuwa unafaa kabisa”.


Katika jibu lake , Kiongozi wa Republican bungeni Kevin
McCarthy amesema : ” ilitokea Pelosi akawa Spika wa bunge hili ,
lakini hazungumzi kwa niaba ya Wamarekani inapokuja katika suala hili
.”
“Hawezi kuamua peke yake kuwa tutakuwa katika upelelezi ,” alisema.
Wakati
huo huo , kaimu mkurugenzi wa shirika la taifa la ujasusi nchini
Marekani , Joseph Maguire, amekataa kushirikisha bunge la Congress
ripoti ya mtu aliyefichua taarifa za shutuma dhidi ya Trump.
Anatarajiwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya umma ya ujasusi siku ya
Alhamisi.

Ni nini kitakachofuata?

Tangazo
la Bi Pelosi linatoa ruhusa rasmi kwa kamati kuchunguza mazungumzo
ya simu za rais wa Marekani na kiongozi wa Ukraine l na kubaini ikiwa
alifanya kosa linaloweza kusababisha afanyiwe uchunguzi wa kumondoa
madarakani.
Katika tangazo lake Bi Pelosi alisema kuwa kamati
nyingine sita zinazofanya uchunguziwa masuala mengine dhidi ya Trump
nzitaendelea na uchunguzi wao chini ya uchunguzi wa sasa.
Ikiwa uchunguzi huu utaendelea, Bunge la wawakilishi litapigia
kura mashtaka yoyote yatakayobainika na kwasababu Democrats ndio
wengi katika bunge la congress wanaweza kupitisha umuzi wa kumshtaki.
Hata
hivyo maamuzi hayo yanaweza kupelekwa katika bunge la Seneti ambako
theluthi tatu ya wabunge inahitajika kupitisha maamuzi – na huko
Republicans wataweza kuzuwia mashtaka.
Kura ya maoni
iliyoendeshwa na shirika la A YouGov ilisema kuwa 55% ya Wamarekani
wangeunga mkono kushtakiwa kwa Trump ika ingethibitishwa kwamba Trump
alisitisha msaada wa kijeshi kwa ukraine ili kuwashinikiza maafisa wa
nchi hiyo kumchunguza Joe Biden.