Wanafunzi wamuua mzee wa miaka 80 kwa tuhuma za uchawi

Mzee Issa Pela enzi za uhai wake

Mzee Anaekadiliwa kuwa na miaka zaidi ya 80 Auwawa na Wanafunzi kwa tuhuma za Ushirikina

Mzee
Issa Pela Mkazi wa Kijiji cha uganga wilayani makete mwenye umri wa
miaka 80 amefariki dunia baada ya shambulio la fimbo kutoka kwa
wanafunzi wa shule ya msingi kwa tuhuma za uchawi ambao unaaminiwa
kusababisha walimu na wanafunzi kudondoka na kuzimia.

Kwa mijibu
wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi luganga Eliuda Msigwa mapema  asubuhi
majira ya saa nne octoba 28 mzee issa alifika shuleni hapo na kuanza
kufanya matukio yanayoashiria vitendo ya ushirikiana ikiwemo kuchora
misalaba chini ya ardhi na kuchuma majani na ndipo wanafunzi wachache
wanaofikia 15 kwa idadi wakaanza kumshambulia kwa kutumia fimbo mpaka
mauati yakamkuta.
Mtendaji wa Kijiji cha uganga ameeleza kuwa
Kijiji hicho kinazungukwa na idadi kubwa ya watu wanaotuhumiwa na
ushirikina hali mabayo inawakwamisha shughuli za maendeleo ikiwemo
ustawi wa elimu ambapo mpaka kufikia tukio la ushambuliwa mzee huyo
shughuli za masomo zilikuwa zimesimama kutokn na walimu na wanafunzi
kukumbwa na vitisho mbalimbali ikiwemo kudondoka na kuzimia ovyo kwa
wanafunzi.

Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo wakiwemo waliohusika
na tukio hilo wamesema kuwa baada ya kumcharaza kwa fimbo mzee huyo
alikiri kuhusika na vifo vya watu watatu kijijini ambao aliwaloga na
baadae mauti yakamkuta kutokana na kichapo.

Mganga mfawidhi wa
zahanati ya Uganga Frank Gavana amethibitisha kutokea kifo hicho baada
ya kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu ambapo amesema majeraha ya
sehemu za kichwa cha marehemu ni sababu kubwa iliyopelekea kifo chake.

Jeshi
la polisi wilaya ya Makete limefika eneo la tukio na kutoa elimu kwa
jamii na kuonya tabia za kuchukua sharia mkononi ambapo hata hivyo
halijamkamata mtu yeyote kuhusika na mauaji hayo

Juhudi za
kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Hamisi Issa kuzungumzia tukio
hilo zinaendelea ambapo awali kwa njia ya simu alisema taarifa hizo
hazija mfikia