Na Mwandishi wetu,Ngorongoro
Watanzania wanaotembelea Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kujionea vivutio vya Utalii, wameongezeka kutokana na uhamasishwaji mkubwa unaoendelea kufanywa na serikali na wadau wengine.
Akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbali mbali jijini Arusha, walioshiriki shindano la Ngorongoro Challenge, walipotembelea Mamlaka hiyo, Mkuu wa masoko katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,(NCAA) Michael Makombe kumekuwepo na ongezeko kubwa la watalii wa ndani.
Alisema tofauti na miaka iliyopita, kwa sasa kumeanza kuibua mwako wa watanzania kutembelea hifadhi, hasa siku za mwishoni mwa wiki na wakati wa siku kuu za kitaifa.
Alisema kujitokeza kwa watalii wa ndani kumetokana na viwango nafuu kwa watanzania ambapo wanalipia kiasi cha sh 11,800 tu kwa watu wazima kuingia hifadhini na gharama ya gari ni sh 20,000 tu”alisema
Wakizungumzia hamasa hilo ya watanzania, John Lyamulya na Walda Caros walisema ni aibu kwa watanzania kushindwa kutembelea hifadhi za taifa na kujionea rasilimali zao ambazo mungu amewapa.
“natoa wito tujenge tabia ya kutembelea vivutio vyetu, kujionea maajabu hasa ya hapo Ngorongoro ambayo hakuna sehemu nyingine duniani”alisema Lyamulya
Walda Caros alisema baada ya kutembelea hifadhi hiyo,amejifunza vitu vingi ambavyo hakuwahi kuvijua katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na akatoa wito watanzania hasa vijana kujitokeza kutembelea hifadhi hiyo.
Elias Metele mmoja ya waongoza watalii, katika makumbusho ya Olduvai alisema Tanzania imebahatika kuwa na utajiri mkubwa wa mambo kale tofauti na nchi nyingi duniani.