Waziri jafo awataka wakurugenzi wasiotimiza ukusanyaji mapato kujitathimini.

Na.Faustine Galafoni.Dodoma.

Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ma Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mh.Selemani Jafo amewataka wakurugenzi wasiotimiza lengo la ukusanyaji
mapato katika Halmashauri zao kujitathimini.

Waziri
Jafo ameyasema hayo    Oktoba 21,2019 Jijini Dodoma  wakati akitoa
taarifa ya mapato ya vyanzo vya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha
Mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2019. .

Waziri
Jafo amesema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa pamoja katika
kipindi hiki imeonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa
ukusanyaji mapato kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi
Bilioni 13.10,huku Mapato ya ndani kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato
Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kukusanya kiasi cha Shilingi
Bilioni 39.53

Pia
Waziri Jafo amesema licha ya Serikali kuagiza ukusanyaji wa mapato
kufanyika kwa njia ya kielektroniki lakini bado kuna Changamoto kwani
kuna baadhi ya maeneo wanakusanya fedha na hawazipeleki benki hivyo
kuwaagiza wakuu wa mikoa kusimamia suala hilo.

Ikumbukwe
kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imekuwa ya mwisho
katika pato ghafi kwa kukusanya Milion 35 kwa kipindi cha miezi mitatu
na hivyo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja wengine ambao
hawajafanya vizuri kujitathimini huku uchambuzi ukionesha kuwa katika
kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20,Jumla ya
Halmashauri 54 kati ya Halmashauri 185 zimefanya vizuri kwa kukusanya
mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 25 ya makisio ya mwaka wa Fedha
2019/20.