Waziri jafo awataka wakuu wa shule kutojihusisha na udanganyifu wa mitihani.

Na  Faustine Gimu
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)
SELEMANI JAFO  amewataka wakuu wa shule za msingi kutojihusisha na suala
la udanganyifu wa mitihani kwa kuwa linaporomosha elimu ya Tanzania.

 
Waziri
Jafo ametoa agizo hilo  jana jijini Dodoma wakati akifungua mkutano
mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania
Bara.
 
Amesema
wao wanadhamana kubwa katika kusimamia sekta ya elimu nchini hivyo
ikitokea uvujaji wa mitihani hauleti picha nzuri katika Taifa.

Akizungumzia
suala la elimu bila ya malipo amesema matumizi ya fedha hizo
yameimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo walipoanza ambapo kulijitokeza
changamoto mbalimbali.

Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi
Tanzania bara(Tapsha), REHEMA RAMOLE ameipongeza serikali kwa uboreshaji
wa miundombinu jambo ambalo limepunguza msongamano wa wanafunzi
darasani.
 
Kauli mbiu ya mkutano huo inasema Uwajibikaji na Usimamizi makini wa Rasilimali katika elimu ndio Msingi wa Elimu Bora.