****
Zaidi
ya shilingi Milioni 154 zimetumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa
na kukarabati shule ya Msingi Luagala ‘B’ Wilayani Tandahimba
Akizindua
madarasa hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba amesema
madarasa hayo yamewekwa na madawati tayari kwa wanafunzi kuendelea na
masomo
“Tumezindua madarasa haya lakini pia wametukabidhi shule
ikiwa katika muonekano unaovutia ambapo kazi hii imefanywa na taasisi
ya Eclat na Upendo ,”amesema Waryuba
Naye Mwenyekiti wa taasisi
ya Eclat Toima Kiroya ameeleza kuwa katika mradi huo wameweza kujenga
vyumba vitatu vya madarasa,kukarabati majengo 8,kisima chenye ujazo wa
Lita 150,000,matundu 16 ya Choo,madawati 65,meza za walimu 16 na viti 16
Hata
hivyo Dk Fred Heimbach wa Upendo Society kutoka Ujerumani ameeleza kuwa
madhumuni ya ushirika huo ni kuboresha miundo mbinu katika sekta ya
elimu
Sambamba na Hilo Meneja wa mradi huo Msham Bashir
ameishukuru serikali kwa kushirikiana kuanzia ngazi ya Kijiji hadi
Wilaya hivyo wananchi wanajukumu lankutunza miundo mbinu hiyo.