Mvua zinazoendelea kunyesha zaleta maafa dodoma

Zaidi ya nyumba 120 zimebomoka na madaraja kuharibika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


Maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ni Bahi Sokoni, Bahi Misheni, Mji mpya, Nkogwa, Mbuyuni, Uhelela, Laloi, Mugu na Nagulo.

Juzi
Mkuu wa Wilaya, Mwanahamisi Mukunda akiongozana na wataalamu wa
Halmashauri ya Bahi na watendaji wa vijiji, walitembelea baadhi ya
wakazi walioathirika na mafuriko hayo na madaraja ambayo yameharibika.

Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kijiji cha Sokoni, Sifael Mbeti
alisema mvua imesababisha mito mingi kufurika na hivyo kusababisha maji
kuleta madhara kwa kubomoa nyumba na madaraja.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bahi Sokoni, Fredrick Kachiwile alisema zaidi ya nyumba 86 katika kijiji hicho zimebomoka.

Alisema
katika Kijiji cha Uhelela taarifa za awali zinaonyesha nyumba 35
zilibomoka na katika Kijiji cha Nagulo barabara imekatika na mawasiliano
ni ya shida.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nagulo, Ashery Silla alisema jumla ya nyumba 18 zimeanguka.