Rais magufuli ashangaa papai, fenesi na mbuzi kukutwa na corona…ashtukia mchezo wa ajabu

CORONA
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ameeleza kushangazwa kufuatia sampuli za Papai, Mbuzi kukutwa
na Virusi vya Corona baada ya kupimwa kwenye Maabara kuu ya Taifa.


Rais Magufuli amesema hayo wakati
akimuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba Chato mkoani
Geita ambapo amemtaka kwenda kufanya uchunguzi kwenye suala la maabara
ya Taifa.

“Waziri nimekuapisha leo itabidi wewe
kwa kushirikiana na Wizara ya Afya mkafanye uchunguzi kwenye masuala
flani katika maabara ya taifa ya Tanzania iliyokuwa inahusika kupima
Corona kuna Controlversal nyingi za ajabu,tuliona walikuwa wanatoa
matokeo chanya..positive positive tu mara nyingi.



Nilizungumza na vyombo vya ulinzi na
usalama na nikatoa maelekezo,hebu nendeni mkacheki hivi vipimo
vikoje,hivyo vifaa vikoje na mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kwamba si
kila kitu unachopewa lazima kiwe kizuri..wanaweza kutumika
watu,vinaweza kutumika hivyo vifaa lakini pia hii inaweza kuwa sabotage
tu kwa sababu hii ni vita”-
Amesema Rais Magufuli.


Ninamshukuru sana Katibu Mkuu Mpya Prof. Mchembe ,wameenda na kufanya mambo yafuatayo kwa kutumia na vyombo vyetu pia:

“Tulichukua Sample za
Mbuzi,tukachukua sample za kondoo,tukachukua sampo za papai,tukachukua
sampo za Oil ya gari na sample za vitu vingine mbalimbali tukavipeleka
pale kwenye Maabara bila wao kujua na tukazipa majina..Sample ya Oil
iliyotoka kwa gari tuliipa jina la Jabir Hamza mwenye miaka 30,ile
ilileta Negative,tulipoleka sample ya Fenesi ambalo tulilipa jina la
Sarah Samwel (45) matokeo yake yalikuwa Unconclusive,tulipopeleka sampo
ya papai tukalipa jina la Elizabeth Anne (26) papai lile lilikuwa
positive maana yake lilikuwa na Corona.


“Tulipeleka sample ya ndege Kware
majibu yakawa positive,tumepeleka Sungura ikawa Undetermined,tumechukua
mbuzi akawa Positive,tukachukua kondoo akawa Negative nk.
Sasa umepeleka sample ukamwambia huyu
ni binadamu halafu ikaleta positive kwamba ina Corona maana yake yale
mapapi yote yale yangewekewa Isolation,ukipeleka mbuzi wa sample nao
wakawa positive maana yake mbuzi wote tulionao au huyo aliyepelekwa naye
apelekwe Isolation,ukipeleka Fenesi likawa positive maana yake makamasi
kamasi yake yale ambayo tuliyapa jina la Elizabeth nayo mafenesi
yalitakiwa yawekwe Isolation”,
ameeleza Rais Magufuli.

“Kwa hiyo ukishagundua hivi lazima
ujue kuna mchezo wa ajabu unafanyika kwenye vipimo hivi…kwamba kuna
mambo ya ajabu yanafanywa katika nchi hii..Either Wahusika wa Maabara
‘Laboratory’ ile wamenunuliwa na Mabeberu,Either hawana utaalamu which
is not True kwa sababu maabara hii imetumika sana kwenye magonjwa
mengine!, Either zile sample zinazoletwa kwa sababu mpaka Reagent
zinatoka nje,mpaka zile Swap..vile vipamba vinatoka nje..lazima kuna
kitu flani kinafanywa

Na kama mapapai yanaonekana Positive
yana Corona basi WHO inatakiwa ifanye kazi kubwa katika haya,na kama
mbuzi nao wana Corona,na kama hawajajua kuwa hii Corona ina affect
binadamu,mbuzi hata miti basi wanasayansi hatujafanya cha kutosha katika
hili…Kwa hiyo kutokana na taarifa hizi zilizonazo lazima  kuna watu
wameambiwa Positive wakati siyo wagonjwa wa Corona na inawezekana
wengine wakafa kwa hofu..Papai lile lipo halijafa, lipo tu linaiva,
mbuzi yule yupo tu wala hajafa, fenesi lile lipo labda lije lioze tu kwa
muda wake lakini yale ni Positive na vitu vingine”,
ameongeza Rais Magufuli.

Kutokana na hali hiyo Rais Magufuli amesema licha ya kwamba Corona ipo amewataka Watanzania kutokuwa na hofu kutokana na Corona