Rc mndeme aipongeza smaujata mkoa wa shinyanga

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme
amewahimiza viongozi wa kampeni ya shujaa wa Maendeleo na ustawi wa jamii
Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga kutekeleza majukumu yao bila kujali
changamoto wanazokutana nazo.

Ameyasema hayo  Februari 27, 2024 kwenye kikao cha pamoja
ofisi kwake ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili namna bora ya kukabiliana na matukio
ya ukatili yanayojitokeza kwenye taasisi mbalimbali, shule na kwenye jamii.

RC Mndeme amewapongeza viongozi wa SMAUJATA kwa
utekelezaji wao wa majukumu huku akiwasisitiza kuendelea kufanya kazi  kwa kujitoa ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa na serikali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili.

Mndeme ametumia nafasi hiyo kuitaka jamii kuwa na
hofu ya Mungu katika maisha ya kila siku na kwamba hatua hiyo itasaidia kuepuka
kutenda matendo ya ukatili katika familia na jamii kwa ujumla.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wamesema
wataendelea kuisaidia serikali kwa juhudi katika kupambana na ukatili ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha viongozi hao pia wamefanya mazungumza ya
pamoja na katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo ambapo kikao
hicho pia kimehudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi na
maafisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga.
SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini inayotekeleza majukumu yake chini ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalum na kwamba kampeni hiyo inaongozwa na shujaa Sospeter Bulugu Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa.Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akiitambulisha kampeni ya SMAUJATA kwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.