Tcra arusha yakutanisha walemavu wa macho, kusikia, juu ya usajili wa laini za simu

Mkuu wa wilaya ya
Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na watu wenye mahitaji
maalumu,kuilia kwake ni Philipo Meli Mwenyekiti wa watu wasioona mkoa wa
Arusha ,kushoto kwake ni Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya ya
kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na wa kwanza mulia ni
Katibu wa chama cha Viziwi Tanzania tawi la Arusha .Picha na Vero
Ignatus.
MHANDISI
Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu
wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona
 Julius
Felix Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini kanda
ya Kaskazini TCRA ,wengine ni washiriki wa semina hiyo ya siku moja
iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwaajili ya kuwajengea uelewa juu ya
usajili wa laini za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.
Jan Kaaya ni Mhandisi Mwanadamizi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA).Picha na Vero Ignatus
Baadhi
ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus
MHANDISI
Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu
wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona katika ukumbi wa
mkuu wa mkoa Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus.
 Baadhi
ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi
ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
 Mhandisi
Imelda Salum Mkuu wa kanda ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini
TCRA akizungumza katika uzinduzi wa semina hiyo ya siku moja ya wadau wa
mawasiliano ,kutoka makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutoona.Picha
na Vero Ignatus.
Mmmoja
wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu
kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa
na TCRA Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Mmmoja
wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu
kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wasiku moja ulioandaliwa
na TCRA Mkoani Arusha.Pcha na Vero Ignatus
Baadhi
ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
.Picha na Vero Ignatus.
Mmoja
wa wakalimani wa lugha ya aklama akisaidia ujumbe ufike kwa waandaaji
wa semina ya watu wenye mahitaji maalum (TCRA).Picha na Vero Ign
atus

Na.Vero Ignatus,Arusha 
Mamlaka
ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini imefanya mkutano wa
siku moja na wadau wa mawasiliano wenyenye mahitaji maalumu, wakiwa
katika makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutokuona.

Lengo
haswa la mkutano huo ni kutoa uelewa kwa watu wenye mahitaji maalum,
kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya mfumo wa alama za
vidole ,pia kuangalia changamoto mbalimbali walizonazo katika huduma za
Mawasiliano

 Gabriel Daqqaro ni
mkuu wa wilaya ya Arusha amesema kuwa semina hiyo itasaidia
,ukizingatia kwasasa kuna changamoto nyingi za mitandao japo kuwa  zipo
faida zake kama vile kupashana habari,kuelimisha,kuburudisha na kukataza
yale mambo mabaya katika jamii katika maendeleo yanayokwenda kwa kasi.

Amesema
kuna makosa ya uhalifu wa kimtandao ,watu wasiowaaminifu wanaotuma
jumbe za kulaghai wa wananchi,kwasababu hiyo serikali imeelekeza  laini
zote za simu zisajiliwe kwa alama za vidole ,hivyo ameipongeza TCRA kwa
kuona watu wenye ulemavu kuwa ni sehemu ya jamii.

Watu
hawa wenye mahitaji maalumu wananchwa mara nyingine kutokana na baadhi
ya watu kudhania kwa mawazo yao hasi kwamba ulemavu ni hasara,niseme
hujafa huijaumbika,nisisitize hebu tubebane tonane tupo sawa.

Daqqaro
amesema serikali ya awamu ya tano imeona hilo, ndipo ikaona watu wenye
mahitaji maalum ,walikuwa hawajajumuishwa katika kunufaika na zile 10%
za mapato ya ndani ,kuanzia mwaka 2018 imetoa maelekezo kwamba na
wenyewe ni miongoni mwa kundi linalotakiwa kunufaika ,ambapo
 halmashauri zote zimeelekezwa hivyo .

Amesema ni muhimu kusajili line za simu ili kuepusha makosa ya uhalifu wa kimtandao, matapeli wanao tuma jumbne
 Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha amesema
serikali serikali iliagiza kuwa 10%za mapato nao watu wenye ulemavu
wanufaikike na mapato ya ndani iliagiza laini zote za simu zisajiliwe
kwa mfumo wa alama za vidole hivyo watu wenye uhitaji maalumu nao ni
sehemu ya jamii.

MHANDISI Imelda Salum ni
Mkuu wa kanda ya kaskazini(TCRA) amesema kuwa Mamlaka hiyo imeamua
kwasababu wao nao ni sehemu ya jamii ,na pia wanatumia huduma ya
mawasiliano hivyo .wanahaki ya kupata taarifa mbalimbali,mafunzo.

“Tunafahamu
kwa namna walivyo wenzetu wana changamoto mbalimbali yumkini kuna
wengine hawawezi kupata taarifa kwa wakati ,lakini kwa wenzetu wa kwa
wasiosikia taarifa kwa taarifa zinazopelekwa kwa jamii kwa njia ya 
radio,televisheni,asiyeona hawezi kuona kwenye televisheni,halikadhalika
asiyesikia vileviel

TCRA
imesema kwa kuona umuhimu wa kundi hilo wameamua kuwashirikisha Mamlaka
ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)ili waweze kutoa huduma kwa watu hao
wenye mahitaji maalum

Mkuu
huyo wa  kanda ya amesema Swala la usiri na faragha kwa watu wasioona
bado limekuwa ni tatizo ,mawasiliano yao yanaweza kutatuliwa tu endapo
kuna vifaa maalumu ambavyo wanaweza kuvitumia zikiwemo simu za mkononi
,pale mtu anaposoma ujumbe aweze kusikia sauti ujumbe unasemaje.

”Ila
mamlaka ya mawasiliano tunajitahidi kuona ni kwa namna gani tunaweza
kuwasaidia ,kwa wenzetu wasioona tunawapa taarifa mbalimbali kupitia
vitabu ambavyo vimechapiushwa kwa zile alama zao maalum.”

Ameainisha
kuwa kila mmoja aone umuhimu wa kujisajili ni kwani watakaposajili
kutumia alama za vidole taarifa zao zinafahamika ,sambamba na kuimarusha
usalama wanapotumia mawasiliano.

Ametoa
wito kwa jamii kulitilia uzito swala hili la kusajili laini,na kwa wale
ambao hawajapata kitambulisho cha NIDA,Mamlaka husika itawasaidia
kupata namba zao,sambamba na wale ambao hawajajiandikisha NIDA wapo
tayari kwaajili ya kuwasaidi ili wajiandikishe wapate kitambuluisho cha
taifa.
Philipo Meli ni
mwenyekiti wa wasioona mkoani Arusha amesema wanaishukuru TCRA kwa
kuwathamini na kuwapatia semina hiyo ya kuwajengea utaalamu na kuwapatia
vitabu vya nykta nundu kwaajili ya kujisomea na kupata uelewa kuhusiana
na mamlaka hiyo ya mawasiliano.

Amesema
katika mawasiliano watu wasioona changamoto kubwa ni mtu wa kuwasomea
ujumbe lazima awepo,hakuna usiri,tunaomba serikali itusaidie uwepo wa
simu ,ambazo tunaweza kusoma ujumbe kwa kusikia sauti ,na iwe katika
lugha ya kiswahili ambapo itaweza kuondoa utegemezi kwa kiwango kikubwa.

“Changamoto
kubwa mtu anakutumia ujumbe hata kama unataka uwe wa siri,inashindikana
mpaka utafute mtu mwaninifu aweze kukusomea ujumbe wako,hiyo ndiyo
changamoto inayotupata sisi watu tusioona.”Alisema Philipo.