Umeme upo wa kutosha wekezeni pwani katika viwanda

Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu akizungumza na wafanyabiasha, wenye viwanda pamoja na wadau
mbalimbali ( hawapo pichani) wakati wa maonesho ya wafanyabiashara na
wenye viwanda yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Pwani.


Naibu Waziri wa Viwanda , Mhandisi
Stella Manyanya(kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari
alipotembelea banda la Shirika la Umeme nchini, TANESCO, wakati wa
maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda yaliyofanyika katika
viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu akisaini kitabu cha wageni alipotebelea banda la Shirika la
Maendeleo ya Petroli nchini( TPDC) viwanda pamoja na wadau mbalimbali (
hawapo pichani) wakati wa maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda
yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu akizungumza na mmoja wa   wenye viwanda walioshiriki katika
maonesho ya wafanyabiashara na wenye viwanda yaliyofanyika katika
viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu,(kushoto) na mhandisi Stella Manyanya wakipata maelezo kutoka kwa
mfanyabiashara mwenye kiwanda aliyeshiri katika maonesho ya viwanda na
wafanyabiashara yaliyofanyika mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu,(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo ( kulia), wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakijiji(
hayupo pichani) baada ya kushindwa kufika katika Kijiji cha Kitima
wilayani Bagamoyo kilichokubwa na mafuriko,baada ya barabara kuharibika
na kujaa maji kufuatia mvua zinazonyesha katika Mikoa ya Ukanda wa
Pwani.
…………………..
Na Zuena Msuya, Pwani
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu amewataka wafanyabiashara, wenye viwanda na wadau mbalimbali wa
maendeleo kuendelea kujenga na kuwekeza katika viwanda mkoani Pwani kwa
kuwa umeme upo mwingi na wa kutosheleza mahitaji ya viwanda hivyo.
Mgalu alisema hayo Oktoba 17,2019
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya pili ya wafanyabiashara na wenye
viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa
Pwani, ambapo Mgeni Rasmi katika maonesho hayo alikuwa ni Naibu Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, kwa niaba ya Makamu wa
Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
Maonesho hayo yanayofanyika kwa
siku 7, yamewashirikisha wafanyabisha, wenye viwanda pamoja na  wadau
mbalimbali ndani na nje nchini, ambapo zaidi wa washiriki zaidi ya 300
wamejitokeza katika maonesho hayo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu
wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Mhandisi Manyanya aliwahakikishia
wafanyabiashara na wenye viwanda kuwa, Tanzania ni sehemu salama ya
kuwekeza, pia serikali imeweka mazingira rafiki katika uwekezaji na
uwezeshaji wa namna yeyote hususani katika viwanda.
Mhandisi Manyanya pia alisema
kuwa, wafanyabiashara na wenye viwanda wasiwe na wasiwasi juu ya
upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kuwa Tanzania ina miradi mikubwa ya
kuzalisha umeme: Akijata visima vya gesi mkoani Mtwara na Lindi pamoja
na Mradi Mkubwa wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere kwa kutumia maporomoko
ya maji katika Bonde la Mto Rufiji utakaozalisha zaidi ya Megawati
zaidi ya 2000 za umeme mwingi ,wa kutosha na wa bei nafuu. 
Akizungumzia hali ya upatikanaji
wa umeme kwa Mkoa wa Pwani, Mgalu alisema kuwa kwa sasa mradi mkubwa wa
kusambaza umeme katika vijiji 150 unatekelezwa ili kurahisisha
usambazaji wa umeme katika viwanda vitakavyojengwa na vinavyojengwa
katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Vilevile Mkoa wa Pwani utanajenga
kituo cha kupoza umeme cha Uruguni pamoja  kutanua kituo cha kupoza na
kupokea umeme cha Mlandizi na Chalinze ambavyo vitakuwa na njia zake za
kusafirisha umeme kwenda viwandani.
Sambasamba na hilo, kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo pia kitatanulia na kuongezewa nguvu
na kuzalisha Megawati 800 za umeme kwa lengo la kuimarisha na kuboresha
upatikani wa umeme katika wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani.
Alilitaka Shirika la Umeme nchini
(TANESCO), kuendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazji
wa umeme ili kuepuka changamoto ya kukatika umeme pasipo sababu ya
msingi.
Kuhusu malalamiko ya bei ya gesi
yaliyokuwa yametolewa na wenye viwanda, Mgalu alitumia hadhara hiyo
kuwaeleza wenye viwanda na wafanyabiashara kuwa , Shirika la Maendeleo
ya Petroli nchini ( TPDC) limepewa kazi kusikiliza na kujadiliana na
wafanyabiasha na wenye viwanda ili kupata mapendekezo ya kuboresha na
kupunguza bei ya gesi kwa manufaa ya watumiaji na  taifa kwa ujumla.
Serikali ilitenga shilingi Bilioni
17 na Dola za Kimarekani milioni 4, kwa ajili ya usambazaji wa umeme
katika Mkoa wa Pwani na shilingi bilioni 64 kwa ajili ya mradi wa
usambazaji umeme wa Peri Urban katika maeneo 186 mkoani humo, ambapo
mahitaji ya umeme kwa sasa ni megawati 82.
Katika hatua nyingine, baada ya
kushiriki katika ufunguzi wa manesho hayo, Naibu Waziri Mgalu, aliungana
na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Kamati ya
ulinza na usalama ya mkoa huo, kutembelea maeneo ya kijiji cha kitima
wilayani bagamoyo ambayo yamekubwa na mafuriko kufuatia mvua
zinazoendela kunyesha katika Mikoa ya Pwani ya bahari ya hindi ikiwemo
Mikoa ya Dar es salaam na Pwani. 
Ilielezwa kuwa wananchi wanaoshi
katika kijiji hicho kukumbwa na mafuriko kwakuzingirwa na maji hivyo
kuhatarisha usalama wa maisha yao, ambapo serikali ilifanya juhudi ya
kuwaokoa na kuwahamishia katika sehemu salama.
Hata hivyo zoezi la viongozi hao
kufika katika kijiji hicho kilichokubwa na mafuriko hazikuzaa matunda
baada ya maji kujaa na kuharibu barabara na hivyo kushindwa kufika
katika eneo la tukio.