Vitendo vya ubakaji, ulawiti wanafunzi vyashamiri arusha

Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Vitendo
vya ubakaji na kulawitiana kwa baadhi ya wanafunzi  wa kiume wa shule
za msingi jijini Arusha vimeelezwa kushamiri kiasi cha wanafunzi
kushindwa kusoma,ambapo walimu wa shule hizo wameitaka jamii kuunganisha
nguvu ili  kutokomeza matukio hayo yanayosababishwa na utandawazi.

Hayo
yamebainishwa  jijini Arusha na baadhi ya walimu wa shule za msingi
wakati wakipatiwa mafunzo maalumu juu ya vitendo vya ukatili na
unyanyashaji dhidi ya wanawake na mtoto yaliyotolewa na shirika
linalojihusisha na utetezi wa haki ya wanawake na watoto la cwcd la
jijini hapa.
Mmoja ya
walimu hao kutoka shule ya msingi Olasiti, Oliver Mbowe amesema kuwa
pamoja na matukio ya ukatili kuwepo kwa baadhi ya familia ,vitendo vya
kulawitiana kwa wanafunzi wa kiume vimeongezeka kiasi kwamba nguvu kubwa
na ushirikiano kwa jamii inahitajika ili kutikomeza vitendo hivyo.

Matukio mengi hivi sasa ni watoto kulawitiana tunachowaomba wazazi
,walezi na jamii kwa ujumla tushirikiane kufuatilia mienendo ya watoto
wetu kwani haya matukio yanasababishwa na sisi wazazi kufanya ngono
tukiwa na watoto wetu kwenye chumba kimoja cha kuishi” Amesema
Amebainisha
kwamba katika shule ya Olasiti anayofanyiakazi matukio hayo yapo na
watoto wengi wa kiume wanajihusisha na mchezo huo hasa wanapokuwa
wanatoka shuleni ama wanatoroka wakati wa masomo.
Alisema
kuwa utandawazi kwa mtoto  kuangalia picha za ngono,pamoja na wazazi
kushiriki tendo la ndoa katika chumba kimoja cha kuishi ni moja vyanzo
vya mtoto kujifunza tabia hiyo mbaya.
Kufuatia
kushamiri kwa vitendo hivyo shirika linalojihusisha na utetezi wa mtoto
na wanawake la cwcd,limeamua kutoa semina kwa walimu ,viongozi wa dini
na viongozi wa makundi mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha juu ya
matukio ya ukatili na unyanyasaji .
Mkuu
wa wilaya ya Arusha,Gabriel Dagarro amesema kuwa serikali ya wilaya kwa
kushirikiana na vyombo vya dola imejipanga kuhakikisha matukio ya
unyanyasaji,ubakaji ,ulawiti na ukatili hayaishii kwa kupatana bali
wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Mkuu
huyo amewataka wazazi na walimu kutoshiriki maelewano na watuhumiwa
badala yake wawe mstari wa mbele kutoa taarifa polisi,ofisini kwake na
ofisi zingine za serikali ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa na hatimaye
kukomesha vitendo hivyo.